TULIYONAYO:

Penzi la Rayvanny na Fahyma lipo pale pale, mashabiki waonya kuhusu kiki



Hivi karibuni kulikuwa na drama za hapa na pale kuwa msanii wa muziki Bongo, Rayvanny ameachana na Baby Mama wake, Fahyma lakini hilo limekuja kuonekana kutokuwa na ukweli wowote mara baada ya msanii huyo kutoa video ya wimbo wake ‘Safari’ ambapo ndani yupo Fahyma.

Licha ya video hiyo kuthibitisha kuwa penzi bado lipo pale pale, Rayvany pia amepigilia msumari katika hilo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amendika; “Sikukupata kwa Bahati Mbaya Kwanini Nikuache kwa Makusudi NAKUPENDA MAMA,”.

No comments