Zaidi ya vijana 100 wanufaika na mafunzo ya ujasiriamali Arusha
Zaidi ya vijana 100 wamepatiwa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa na Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa (FJS), yenye lengo la kuwapatia vijana elimu ya kujiajiri ili kujikomboa kiuchumi.
Mkurugenzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali Joseph Mayagila amesema tangu mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo hutolewa kila mwaka kati ya vijana 570 waliopatiwa mafunzo zaidi ya vijana 260 wameanzisha biashara zao wenyewe.
Mayagila amesema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji fanikiwa kilichopo kwa morombo jijini Arusha.
“kupitia mafunzo haya yatakufanya na wewe ujitambue na ujielewe na mjitambue kiuchumi hamtakuwa tena tegemezi kwenye familia zenu na hata mtakaporudi majumbani kwenu mtawasaidia wazazi wenu wakafanya vizuri hatakama wazazi wako ni wafugaji kwa mawazo uliyonayo utawasaidia baba na mama kuwakuza kiuchumi,” alisema mayagila
Pamoja na mambo mengine, mayagila amesema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kuzitumia fursa zinazowazunguka na kutumia fursa hizo kwa kuchanganya na juhudi zao binafsi kwa kuanzisha miradi ya biashara ambayo itakuwa endelevu na kuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe pamoja na kuwaajiri vijana wengine.
Kwa upande wake Andrew Ngobole ambaye ni mkuu wa chuo hicho na mkufunzi katika mafunzo hayo, amewataka washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali kuzingatia muda na matumizi bora ya fedha katika biashara zao.
“Muda na kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha ni jambo muhimu katika kufanya biashara kama hukuweza kuyazingatia haya unaweza ukasema biashara ngumu au ukitumia fedha ya biashara bila kuwa na nidhamu nayo unaweza ukafilisika kwa kuyumba kwa mtaji,” alisema ngobole.
Ahazi ngesi, ni mkurugenzi wa mradi wa KUKU UCHUMI pia ni mkufunzi katika semina hiyo amewaasa vijana kujishughulisha na ufugaji wa kuku kwani unazaidi ya biashara miatano ambazo zitawakwamua vijana kiuchumi.
“wewe kama kijana ukishajiingiza katika biashara ya kuku umasikini umeuaga, mradi wa kuku unaabiashara nyingi tatizo wakuzichangamkia ndio hawapo kwenye kuku kunazaidi ya biashara kumi na tano ambazo unaweza kuzifanya kutoka kwa kuku tu"alisema ngesi.
kwa upande wao wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo hayo wamekiri kupata elimu mpya ambayo itawasaidia kujiajiri wao wenyewe na kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi katika familia zao.
Mafunzo ya Ujasiriamali hutolewa kila mwaka katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji fanikiwa yakiwa na lengo la kuwakwamua vijana kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea kibiashara.
No comments