CHADEMA wakamatwa mkoani Kilimanjaro.
Leo september 20 Viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Kilimanjaro akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Owenya, wamekamatwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na kupelekwa kituo cha polisi cha Bomang’ombe.
Lucy na viongozi wengine, wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya siasa katika ya shule ya Sekondari ya Rundugai wilayani humo na kufanya siasa kinyume cha utaratibu.
Wengine waliokamatwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu, Katibu wa Mbunge wa Hai, Irene Lema na Diwani wa Machame kaskazini, Clement Kwayu.

No comments