Mitandao ya kijamii itazamwe kama fursa ya ajira Tanzania.
Na Francis Masirory
Wakati malalamiko ya changamoto zitokanazo na matumizi ya mitandao ya kijamii zikizidi kuongezeka hasa katika mmomonyoko wa maadili bado kuna fursa katika mitandao ambazo hazitumiwi ipasavyo.
Hayo yameelezwa leo na mkufunzi wa mafunzo ya ujasiriamali Bw Onesmo elia mbise katika mfululizo wa mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji fanikiwa.
Mbise amesema ni vyema vijana wakatumia mitandao ya kijamii kujitangaza na kutengeneza fursa za ajira jambo ambalo litawakutanisha na wadau wenye mahusiano na kazi wanazozifanya ili kujitengenezea fursa za ajira.
“Tuanze na mitandao ya kijamii kujitangaza na kutangaza kazi zako ili wadau wenye mahusiano na kazi zako waone kazi unazozifanya ukiposti picha kunawatu wanao kutazama kwa mitazamo tofauti utapata likes na comments either nzuri au za kejeri usikate tamaa simamia katika kile unachokifanya” alisema mbise.
Sambamba na hayo mkurugenzi wa mafunzo hayo Bw joseph mayagila amesema kuwa vijana wengi wanaingia katika biashara bila ya uelewa mpana wa kibiashara na kutambua namna ya kukabiliana na ushindani wa masoko jambo ambalo linapelekea biashara nyingi kufa.
Aidha mayagila ameendelea kwa kuwaomba wafanyabiashara kupunguza gharama za kibiashara ili kuweza kuendesha vyema shughuri zao za kibiashara.
“kiongozi wa kibiashara lazima ajifunze kupunguza gharama za kibiashara kama hauwezi kupunguza gharama za kibiashara hauwezi kusimamia biashara, lazima upunguze gharama za uendeshaji wa biashara” alisema mayagila
Kwa upande wao wanafunzi ambao wamekuwa wakihudhuria mafunzo hayo wamesema wamenufaika na mafunzo hayo jambo ambalo litawasaidia kuepukana na zana ya kutegemea kuajiriwa na badala yake watakuwa na uwezo wa kuzigundua fursa na kujiajiri wao wenyewe.
Mafunzo hayo yamekuwa na faida kubwa kwa wanaodhuria na yalifunguliwa juma tatu ambapo leo ni siku ya tatu huku kilele cha mafunzo hayo kinatarajiwa kuwa ni siku ya ijumaa.

No comments