Binti mtanzania mwenye umri mdogo kuweka rekodi ya kupanda mlima Everest
Na:Francis masirory
Binti Mtanzania mwenye asili ya bara la Asia Rawan Dakik (18) aliye panda milima 19 maarufu duniani anatarajia kuandika rekodi ya dunia kwa kuwa binti wa kwanza Mtanzania kuupanda mlima Everest.
Akizunguma na bonganasi blog nyumbani kwao jijini arusha lisema alianza kupanda mlima kilimanjaro akiwa na umri wa miaka 11 na hadi sasa amefanikiwa kupanda mlima huo Zaidi ya mara tatu.
Dakik anatarajia kupanda milima Everest, mlima mrefu zaidi duniani ifikapo mwezi mach 2020, na huutumia mlima Kilimanjaro kama sehemu yake ya mazoezi katika kufanikisha kuupanda mlima Everest.

No comments