Mhariri wa gazeti ayatuhumu makanisa ya Ujerumani
Mhariri wa moja ya magazeti yanayoongoza hapa Ujerumani
ametawala mitandao ya kijamii baada ya kutoa kauli ya kutuhumu mahubiri
ya Krismasi kwamba yalikuwa na upendeleo wa siasa za mrengo wa kushoto.
Mhariri mkuu wa gazeti la Die Welt, mojawapo ya magazeti yanayoongoza nchini Ujerumani na lenye mtazamo wa kihafidhina, amechochea mjadala katika mitandao ya kijamii wakati wa Krismasi baada ya kulalamika kwamba mahubiri yalikuwa ya upendeleo kwa mirengo ya kushoto katika misa ya usiku ya Krismasi.
Ulf Poschardt aliandika kupitia ukurasa wake wa twitter katika usiku wa mkesha wa Krismasi kwamba "Nani anaweza kwenda ibada ya usiku kwa hiari ikiwa mwisho wa ibada atajihisi kwamba ametumia siku yake na Jusor au tawi la vijana wa kijani?", akimaanisha matawi ya vijana ya vyama vya Social Democratic SPD na kile cha kijani, ambayo yote yanawakilisha mrengo wa kushoto wa vyama vyao.
Kauli yake ilikuja siku chache baada ya kiongozi wa chama siasa za mrengo mkali wa kulia cha AfD, Alice Wiedel kutoa malalamiko sawa kwa jarida la Focus akisema kwamba makanisa yameingiliwa na siasa.

No comments