Kisonono
ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya
Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka
katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya
kizazi kwa wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa
(urethra), mdomoni na kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea
kwenye shingo ya kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono
hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15-19 wanawake walio katika umri wa
miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 -wako kwenye
hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Ugonjwa huu huambukizwa vipi? Ugonjwa
huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja
kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza
kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum).
Ugonjwa wa gono huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni
kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya
kulevya.Dalili za ugonjwa wa kisonono Dalili
za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7
baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili
ni kama zifuatazo;
Kwa wanaume:
Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation)
Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana
Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
Maambukizi
yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia
haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza
kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.
Kwa wanawake:
Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote
Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu
Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika.
Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa
Kichefuchefu
Homa (fever)
Kutapika
Vipimo vya ugonjwa wa kisonono
Swab
for culture Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria
baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna
bakteria wanaosababisha gono.
Polymerase Chain Reaction (PCR) Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.
Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini? Tiba
ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi
magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na
kama mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye
shingo ya kizazi (cervix), urethra na
Puru,
dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za
aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya
penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara
nyingi kwa wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa
kuchomwa sindano. Fuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi
kwani dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito (mfano doxycyclin).
Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote wawili na ni vizuri wapenzi
wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za ugonjwa huu.Madhara
ya ugonjwa wa kisonono
Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
Huweza kuathiri moyo (heart valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
Madhara kwenye sehemu za maungio au jointi (joint inflammation)
Kwa
wanawake wale ambao hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic
Inflammatory Disease) ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
Wale
wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari
ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake
(preterm labor).
Kwa
wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza
kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo
(meningitis), kuwa kipofu (blindness), homa ya mapafu (pneumonia) na
ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).
Kinga ya kisonono
Kutumia kondomu wakati wa kujamiana
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
Kwa
wanawake wajawazito Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate
kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa
gono au ugonjwa mwengine wowote.
Wanawake
wajawazito wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto
ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha
kuwa kipofu.
Epuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono.
"Kumbuka
ya kwamba hakuna kitu kama ngono salama kwani huwezi kujua kama wewe au
mwenzako wakati wa kujamiana ameathirika au la, au una michibuko au
umekatika kwenye ngozi au la kwani michibuko mengine inaweza isionekane
au kugundulika kwa urahisi. Njia pekee na nzuri ni kuacha au kujikinga
na vitendo vya ngono". Mtu aliyepata gono awali anaweza kupata tena. ummu kulthum Aende hospitali kupiga Sindano haraka iwezekanavyo.
Ifahamu (gonorrhea) kiundani.
Reviewed by bonganasi
on
December 29, 2017
Rating: 5
No comments