George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia
George Weah Leo atatangazwa kuwa
Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo baada ya kuongoza kwa
asilimia 61.5 kati ya kura asilimia 98.1 zilizohesabiwa.
Bwana Weah amemtangulia mpinzani wake Joseph Boakai kwa kura asilimia 60.Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia.
- George Weah kuwania urais Liberia Oktoba
- Ugonjwa usiojulikana wawaua watu zaidi Liberia
"Ninaelewa umuhimu na majukumu ya kazi kubwa niliyokabidhiwa leo. Mabadiliko yanakuja."
George Weah ni nani?
Weah ni mwanasoka maarufu aliyecheza kwenye klabu za soka za juu Ulaya kama Paris St-Germain (PSG) na AC Milan, kabla ya kumaliza taaluma yake nchini Uingereza kwa kuwachezea kwa muda mfupi klabu za Chelsea na Manchester City.Ni Mwafrika pekee aliyewahi kushinda tuzo ya Fifa ya mchezaji bora duniani ya na tuzo ya Ballon D'Or.
- Mwanafunzi mmoja pekee apita mtihani Liberia
- Netanyahu aelekea Liberia kwa mkutano wa Ecowas

No comments